21 Aprili 2025 - 18:05
Palestina lazima ibaki / Watawala wetu wamepotoka kutoka kwenye Misingi ya Umma wa Kiislamu

Mwenyekiti wa Majlisi ya Umoja wa Waislamu wa Pakistan akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuiunga mkono Palestina amesema kuwa, watawala na wanasiasa wa sasa wa nchi hiyo wamejitenga na thamani halisi za Umma wa Kiislamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (AS) - ABNA - Seneta Raja Nasser Abbas Jafari, Mwenyekiti wa Majlisi ya Umoja wa Waislamu wa Pakistan, alisema katika hotuba yake katika Semina ya Karbala ya Zama za Palestina: "Yazid alishindwa jana na atashindwa leo." Anayesimama kwa kanuni na misingi yake, huyo anaishi (yupo hai) na ushindi ni wake.

Amesisitiza kuwa wajibu wetu mbele ya dhulma ni kuonyesha ustahimilivu na kukabiliana na madhalimu na kwamba kuinuka na kupambana dhidi ya dhulma ni wajibu wetu.

Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan aliendelea: Baada ya tukio la A'shura, Wanawake wa Ahlul Bayt (AS) walionyesha ustahimilivu na walianzisha mihanga ya Karbala kwa ulimwengu. Wale wanao jitahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu wana ahadi za Mwenyezi Mungu na malipo makubwa.

Raja Nasser aliongeza: "Adui anajaribu kuharibu upinzani na kuudhoofisha kwa kueneza habari, lakini jukumu letu ni kuhakikisha kuwa upinzani unasalia na unaendelea." Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu kwamba yeyote anayemsaidia, Mwenyezzi Mungu pia atamsaidia.

Aliendelea kusema: "Lazima tuhuishe mwendelezo wa kuiunga mkono Palestina." Watawala na wanasiasa wetu wa sasa hawatokani na Umma wa Kiislamu. Umma wa Kiislamu ni wenye kuamrisha mema na kukataza maovu. Hakuna mnafiki katika Ummah wa Muhammad (S.A.W.W).

Mtu huyu mashuhuri wa Pakistan alihitimisha kwa kusema: "Mashahidi wa Gaza na Palestina wako hai siku zote, kwa sababu shahidi sio tu yu hai, bali analipa taifa uhai." Mfia-imani (Shahidi) anauamsha Umma wa Kiislamu, na Umma uliolala na ulio kimya, lakini (kwa bahati mbaya) Umma unaiunga mkono Israeli.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha